Wednesday, June 12, 2013

0
WIZARA YA ELIMU YATANGAZA NAFASI ZA MASOMO YA UALIMU 2013/2014

 
Nafasi za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Daraja A na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2013/2014.
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anawatangazia Wahitimu wa Kidato cha Nne mwaka 2012 na Kidato cha Sita mwaka 2013 kuwa muda wa kupokea maombi kwa ajili ya mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti na Stashahada mwaka wa masomo 2013/2014 umeongezwa mpaka tarehe 28/06/2013.

Sifa za mwombaji ni kama zilivyoainishwa katika tangazo la Wizara lililopo katika tovuti ya Wizara www.moe.go.tz linalohusu “Nafasi za Mafunzo ya Ualimu Ngazi ya Cheti Daraja A na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2013/2014”.Bofya hapa
 
Aidha, wahitimu wa kidato cha Sita kuanzia mwaka 2008 hadi mwaka 2013 wanahimizwa kutuma maombi yao.
Barua za maombi zioneshe Jina na anuani kamili ya mwombaji na kuambatisha nakala ya matokeo yake ya mtihani (wahitimu wa Kidato cha Nne 2012 na Kidato cha Sita 2013 waambatishe ukurasa wenye matokeo yao kutoka Baraza la Mitihani la Tanzania Au kuonesha namba yake ya mtihani)

Maombi yatumwe kwa:-

Katibu Mkuu,  

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,

S.L.P.9121,

DAR ES SALAAM 

Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

Tupe Maoni Yako( Usiandike Matusi )

0 Maoni: