Saturday, June 01, 2013

0
MWENYEKITI WA CCM KYELA AVULIWA ATIMKIA CHADEMA


ALIYEKUWA Mwenyekiti wa  Kitongoji cha Bondeni  A na makamo mwenyekiti wa Maml aka ya mji mdogo wa Kyela kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Amani Mwaitubi amejiunga na Chama cha Democrasia na maendeleo (CHADEMA), baada ya kutofautiana na maamuzi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM,

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi nyumbani kwake mara baada ya kuchukua fomu yakutaka kukitetea kiti chake kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA )katika uchaguzi utakaofanyika mwezi wa saba mwaka huu alisema kuwa amefikia hatua hiyo baada ya chama cha mapinduzi kumvua uanachama baada ya kukataa kutii matakwa ya chama hicho cha kusaini kupokonya soko la mkibege linalomilikiwa na wananchi wa kitongoji hicho kwenda mikononi mwa chama,

Alisema kuwa soko la mkibege lilianzishwa mwaka 1974 likiwa linamilikiwa na wananchi wa kijiji hicho chini ya muasisi marehemu Said Mwafilombe na kuwa tangu wakati huo hakuwahi kusikia kuwa soko hilo lipo chini ya chama ambapo mwanzoni mwaka huu aliitwa na viongozi wa cama cha mapinduzi wakimtaka akabidhi soko hilo mikononi mwao

Aliendelea kudai kuwa yeye aligoma kufanya hivyo kwa madai kuwa hayupo tayari kuwasaliti wananchi kwa kuwa ndiyo waliompa dhamana ya kuwa mwenyekiti na kuwa kufuatia msimamo huo walimuandikia barua ya kumvua uanachama na hatua hiyo inamnyima nafasi ya kuendelea na wadhifa huo wa uenyekiti wa kitongoji hivyo kuamua kujiunga na Chadema na kupewa kadi mpya yenye namba 0068953 ambapo Chadema ilimpa lidhaa ya kugombea ili kutetea kiti chake,

Katika uchukuaji wa fomu ya kugombea uenyekiti alisindikizwa na mamia ya wananchi wa kitongoji hicho huku msafara ukipambwa na pikipliki zaidi ya 30 ukianzia nyumbani kwalke hadi kwenye ofisi za mamlaka ya mji mdogo huku msafara huo ukiimba nyimbo za kumsifu kiongozi huyo kwa msimamo wa kuwatetea wananchi wa kitongoji chake,

Afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa kyela Bw, Samwe Raphael alikiri kuwepo na hali hiyo na kudai kuwa baada ya Chama cha Mapinduzi kumvua uanachama alipewa taarifa kwa maandishi na y eye alipeleka muhtasari kwa Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela Abdallah Mfaume baada ya kujiridhisha walimuandikia barua ya ukomo wa uenyekiti yenye kumbukumbu na KTA.V.1/06/30 ya tarehe 9 april 2013,

Samwel  alidai kuwa walifanya maamuzi hayo baada ya kutumia kifungu cha 26 kifungu kidogo cha kwanza kinachosemanafasi ya Mwenyekiti wa kitongoji itakuwa wazi na kuitisha uchaguzi mungine endapo aliyekuwepo awe amekufa,kujiuzuru,kuhamia kitongoji  kingine au chama kilichompa dhamana  kumvua uanachama,

Aidha Bw,  Samwel aliongeza kuwa kwa kuwa Chama cha Mapinduzi kimemvua uanachama Mwenyekiti huyo basi yeye kama Afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya mji mdogo wa Kyela TEO alitangaza nafasi hiyo kuwa wazi ndani ya siku saba na katika siku sitini uchaguzi uwe umefanyika ili kumpata Mwenyekiti atakaye ijaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi,

Wengine waliochukua fomu ya kuwania uongozi huo wa kitongoji hadi sasa ni Williamu Lufingo Salumu Kupitia Chama Cha Mapinduzi( CCM)

NA IBRAHIM YASSIN

Tupe Maoni Yako( Usiandike Matusi )

0 Maoni: