Thursday, June 13, 2013

0
INAAMINIKA HIZI NDIZO SABABU ZA KIFO CHA MSANII LANGABaba Langa leo nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar

Baba mzazi wa Langa, Mangisemi Kileo ameeleza chanzo cha kifo cha mwanaye ambacho kimetokea leo katika Hospitali ya Muhimbili.

Langa amefariki dunia leo katika hospitali ya Muhimbili baada ya kulazwa usiku wa kuamkia jana.
 
Hapa ndiyo nyumbani kwao Langa mara baada ya taarifa za msiba wake, leo.
Imeelezwa Langa alifikishwa hospitalini hapo akiwa amezidiwa na moja kwa moja akafikishwa katika chumba cha watu mahututi.

 Mwandishi wa habari hii alifika nyumbani kwao marehemu eneo la Mikocheni Regency dakika chache baada ya taarifa za msiba na kuzungumza na baba yake mzazi, Mengiseni Kileo.
 
Langa
Kileo alisema Langa alizidiwa ghafla juzi, wakamkibiza katika Hospitali ya Kairuki.
 
“Pale walituambia kwamba anasumbuliwa malaria kali pamoja na ugonjwa wa uti wa mgongo.

“Hivyo tukalazimika kumkimbiza Muhimbili ambako alifikishwa katika chumba cha watu matuhuti (ICU), leo ndiyo mauti yamemkuta,” alisema.

Kuhusiana na mazishi, Kileo alisema wanalazimika kumsubiri mkewe, Venus ambaye anatarajia kutua nchini kesho au keshokutwa.

“Mama yake yuko Marekani, hivyo tutamsubiri lakini tumeshazungumza naye.

“Sisi tutakaa leo kujadili suala hilo na wanafamilia na baadaye tutajua kila kitu,” alisema Kileo akionesha utulivu.

Langa alikuwa akitamba na nyimbo yake mpya ya Rafiki wa Kweli iliyotengenezwa katika studio za Bongo Record chini ya P Funk.
 
Msanii huyo alianza kutamba baada ya kushinda usakaji vipaji chini ya Coca Cola na kuunda kundi la Wakilisha akiwa na Shaa au Sarah na Witness wakianza na wimbo wao wa kwanza ‘Hoi’.
 
Credits: salehjembe

Tupe Maoni Yako( Usiandike Matusi )

0 Maoni: